• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uingereza kufunga shule kutokana na COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-03-19 09:52:42

    Waziri mkuu wa Uingereza Bw. Boris Johnson amesema shule zote zitafungwa kuanzia Ijumaa kufuatia mamlaka ya afya ya nchi hiyo kuthibitisha vifo vya watu 104 na mambukizi 2,626 ya virusi vya korona nchini humo.

    Lakini Bw. Johnson amesema watoto wa wafanyakazi wa afya, maofisa wa polisi na wafanyakazi wa sekta nyingine kuu, pamoja na watoto waishio katika mazingira yenye changamoto bado wanaweza kwenda shule.

    Mapema Jumatano, mamlaka ya afya ya Uingereza imesema hadi kufikia Jumatano watu wengine 32 walifariki kutokana na virusi hivyo. Wakati huohuo, serikali za Scotland na Wales zimetangaza kufunga shule kuanzia Ijumaa. Huko Ireland Kaskazini shule zilifungwa saa 11 jana jioni kwa wanafunzi, lakini walimu wataendelea kufanya kazi kwa siku mbili nyingine.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako