• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Chelsea kusaidia wahudumu wa afya wanaopambana na virusi vya korona

  (GMT+08:00) 2020-03-19 16:16:16

  Mmiliki wa klabu ya Chelsea Roman Abramovich amesema Millenium Hotel iliyoko Stamford Bridge itawapokea na kuwapa malazi maafisa wa afya wa serikali wanaopambana na virusi vya korona. Katika taarifa yake, Klabu hiyo imesema mmiliki huyo atagharamia kwa kipindi cha miezi mitatu, lakini ataendelea iwapo maafisa hao wataendelea na shughuli hizo hata baada ya muda huo kumalizika. Amesema ana hakika baadhi ya maafisa hao watakuwa wakifanya kazi hadi usiku na watakuwa na shida ya usafiri. Hivyo wameamua kuwapa makazi kama mojawapo ya mpango wa klabu hiyo wa kujitolea katika vita vya kupambana na ugonjwa huu hatari. Millennium Hotel and Resort ambao ni wasimamizi wa hoteli hiyo watasaidiana na wafanyakazi wa klabu kutoa huduma kwa maafisa hao wa afya.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako