• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Hakuna maambukizi mapya ya COVID-19 mkoani Wuhan, China

    (GMT+08:00) 2020-03-19 17:30:08

    Mkoa wa Wuhan ulioathirika zaidi na virusi vya korona nchini China haujaripoti maambukizi mapya hapo jana, na kuashiria siku ya kwanza kwa mkoa huo kutokuwa na mgonjwa mpya katika miezi miwili ya kupambana na virusi hivyo.

    Tume ya Afya ya Mkoa wa Hubei, imesema idadi ya vifo vilivyotokana na virusi hivyo iliongezeka wa watu wanane, lakini kesi za jumla zilizothibitishwa za virusi hivyo katika mji wa Wuhan na miji mingine ya mkoa huo imeendelea kuwa 50,005 na 67,800 hapo jana.

    Awali, mkoa huo uliripoti ongezeko dogo la maambukizi mapya, ambayo yote yalitokea mjini Wuhan, kwa muda wa wiki moja mfululizo kuanzia jumatano iliyopita, tofauti na mwezi mmoja uliopita ambapo idadi hiyo ilikuwa ni maelfu kadhaa kwa siku.

    Kutokana na kutokuwa na kesi mpya mjini Wuhan, China bara jana ilipunguza maambukizi ya ndani kwa sifuri, wakati nchi hiyo ikikabiliwa na tishio la maambukizi yanayotoka nje ya nchi, ambayo yaliongezeka na kufikia 34 hapo jana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako