• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kesi za maambukizi ya COVID-19 zaendelea kuongezeka barani Afrika

    (GMT+08:00) 2020-03-19 17:44:36

    Hadi kufikia jana, nchi 31 za Afrika zimeripoti kesi zaidi ya 500 za maambukizi ya ugonjwa wa nimonia iliyosababishwa na virusi vipya vya korona COVID-19, na kati ya nchi hizo, Mauritius, Djibouti na Zambia zimeripoti kesi hizo kwa mara ya kwanza. Nchi za Afrika zimechukua hatua mbalimbali kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa huo.

    Wizara ya afya nchini Rwanda imesema, kuanzia kesho, nchi hiyo itasimamisha safari za ndege za kibiashara za abiria kati ya nchi hiyo na nchi za nje kwa siku 30.

    Rais Felix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ametangaza hatua kadhaa za kukinga COVID-19, ikiwemo kusimamisha ndege zote zinazotoka au kupitia nchi zinazoathirika vibaya na ugonjwa huo, kutoruhusu raia wa nchi hizo kuingia DRC, kupiga marufuku mkusanyiko wa watu zaidi ya 20, na kufunga shule, nyumba za ibada na kumbi za burudani.

    Uganda nayo imetangaza kuwa kuanzia jana, abiria wote kutoka Italia, Ufaransa, Korea Kusini, Marekani, Uingereza, Uholanzi, Uswizi, Sweden, Ubelgiji, Hispania, Norway, Austria, Malaysia, Pakistan, na nchi nyingine wanatakiwa kutengwa kwa siku 14 baada ya kufika nchini humo ili kufuatiliwa afya zao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako