• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • WHO yasema si sahihi kulinganisha virusi na mataifa

    (GMT+08:00) 2020-03-19 18:47:35

    Rais Donald Trump wa Marekani hivi karibuni aliviita virusi vya COVID-19 kuwa 'virusi vya China', kutokana na kauli hiyo, mkuu wa Idara ya Matukio ya Dharura iliyo chini ya Shirika la Afya Duniani WHO Bw. Michael Ryan amesema, si sahihi kulinganisha virusi na mataifa.

    Bw. Ryan amesema, virusi havihusiani na nchi, makabila, rangi au fedha, na ni lazima kuepuka kuvilinganisha na mambo hayo. Amesema watu wote wanapaswa kushirikiana kwa pamoja katika mapambano dhidi ya virusi hivyo.

    Bw. Ryan pia amesema, mafua ya H1N1 yaliyoanza nchini Marekani yalilipuka duniani mwaka 2009, lakini hamna mtu anayeita mafua hayo kama mafua ya Marekani. Ameongeza kuwa huu ni muda wa kupambana kwa pamoja dhidi ya virusi hivyo bila ya kulaumiana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako