• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uganda kuachana na pesa taslimu na kuanza matumizi ya pesa kwa nia ya simu kama njia moja ya kujikinga na maambukizi ya COVID-19

  (GMT+08:00) 2020-03-19 19:16:03
  Ijapokuwa hakuna kisa chochote cha maambukizi ya virusi vya COVID-19 nchini Uganda,inaonekana kuwa matayarisho ya kujikinga iwapo kutakuwa na mlipuko yamepamba moto.

  Ili kupunguza maambukizi kupitia pesa taslimu,kampuni ya simu ya MTN ,nchini humo,imeanza hatua ambayo itapunguza ukamataji wa pesa taslimu na watu kufanya miamala na malipo kwa njia ya simu.

  Kulingana na barua iliyoandikwa jana na Afisa Mkuu Mtendaji wa MTN,Bw William Vanhelleputte,kwenda kwa Idara ya Kitaifa ya Mifumo ya Malipo ya Benki Kuu ya Uganda ,majadiliano na Benki Kuu pamoja na benki zingine yalifanyika,na kusababisha ukuzaji na matumizi ya pesa kwa njia ya simu kuliko kukamata pesa taslimu kama njia moja ya kujikinga na maambukizi ya COVID-19.

  Mojawapo ya mapendekeo yaliyoandikwa katika barua hiyo ni pamoja na kutokuwa na ada yoyote kwa miamala isiyozidi Sh30,000.

  Katika hotuba yake wakati akihutubia Taifa siku ya jumatano,Rais Yoweri Museveni alisema Wizara ya Afya itatoa taratibu zinazofaa kuhusu miamala ya pesa,ikiwa ni pamoja na matumizi ya pesa kwa njia ya simu,kufanya manunuzi mitandaoni,miongoni mwa mengine.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako