• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapenda kushikiana kwa kina na nchi za Asia, Ulaya na Afrika kukabiliana na COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-03-19 19:33:28

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Geng Shuang amesema, China inapenda kushirikiana kwa kina na nchi za Afrika, Asia na Ulaya kukabiliana na COVID-19, ili kulinda usalama wa afya ya umma wa kikanda na kimataifa.

    Geng amesema China itatoa uzoefu wake wa kupambana na ugonjwa huo kwa nchi za Afrika bila ya kuficha chochote, na pia itatoa msaada kwa nchi hizo kadiri iwezavyo, ili kushinda ugonjwa huo kwa pamoja.

    Amesema China pia itashirikiana na nchi za Asia na Ulaya kwa kina, ili kulinda usalama wa afya ya umma ya kikanda na kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako