• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Kenya yapewa wito wa kufanya kikao ili kuokoa soka yake

    (GMT+08:00) 2020-03-20 08:26:11

    Aliyekuwa mwenyekiti wa klabu ya AFC Leopards, Alex Ole Magelo ametoa wito kwa wadau wa soka nchini Kenya kukutana haraka iwezekanavyo kupanga mikakati itakayookoa mchezo huo baada ya Jopo la Kutatua Mizozo Michezoni (SDT) kufutilia mbali uchaguzi wa Shirikisho la Soka la Kenya (FKF). Uamuzi huo kadhalika ni nafuu kwa mwenyekiti wa zamani wa FKF, Sam Nyamweya ambaye ni mpinzani mkuu wa Nick Mwendwa ambaye muda wa kamati yake kuwa mamlakani umemalizika. Nyamweya anaungwa mkono na Twaha Mbaraki anayetaka kuwa naibu wake. Kundi hilo limeupongeza uamuzi wa SDT huku likidai kwamba umeokoa soka ya Kenya kwa jumla. Kufuatia uamuzi huo wa Jumanne, Kenya inakabiliwa na hatari ya kupigwa marufuku na FIFA kushiriki katika mashindano ya kimataifa. Hali hii inaiweka mashakani kamati ya Nick Mwendwa ambayo muda wake wa kuwa mamlakani ulimalizika Februari 10, baada ya ule wa nyongeza kufika ukingoni mnamo Januari 26, hii ikimaanisha kundi la Mwendwa halikubaliwi kuhusika na maswala ya soka kwa sasa. Mjumbe wa FIFA, Sarah Salomale aliagiza uchaguzi wa marudio ufanyike kabla ya muda wa maafisa wa sasa kumalizika, huku akisisitiza kwamba lazima bodi itakayosimamia uchaguzi izingatie maagizo na mapendekezo ya SDT.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako