• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • WHO yasema China kutokuwa na mgonjwa mpya wa COVID-19 ni mafanikio mkubwa

    (GMT+08:00) 2020-03-20 09:49:28

    Katibu mkuu wa Shirika la Afya Duniani WHO Bw. Tedros Adhanom Ghebreyesus jana huko Geneva amesema, China kutokuwa na mgonjwa mpya wa COVID-19 kwa mara ya kwanza ni mafanikio makubwa.

    Bw. Tedros amesema, kwa sasa kote duniani idadi ya wagonjwa wa COVID-19 imezidi laki 2, na idadi ya vifo kutokana na ugonjwa huo imezidi elfu 8, lakini kwa mara ya kwanza China kutokuwa na mgonjwa mpya wa COVID-19, ni mafanikio makubwa sana.

    Pia amesema, WHO imetuma vifaa vya kujikinga kwa nchi 68, na kutuma vitendanishi vya kupima COVID-19 kwa nchi 120. Sasa WHO inapanga kuagiza vifaa vya kupambana na maambukizi kutoka kwa kampuni za China. Ameongeza kuwa nchi nyingi zina mahitaji makubwa ya vifaa hivyo, na upungufu wa vifaa bado utakuwa changamoto katika siku za usoni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako