• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa ripoti ya uchunguzi kuhusu masuala yanayomhusu Daktari Li Wenliang

    (GMT+08:00) 2020-03-20 09:50:47

    China imetoa ripoti ya uchunguzi uliofanywa na kamisheni ya Usimamizi ya taifa kuhusu masuala yanayomhusu daktari Li Wenliang, ambaye aliitwa na kupewa hati ya karipio na polisi baada ya kutoa taarifa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kutokea kwa maambukizi ya ugonjwa wa SARS Desemba 30 mwaka jana mjini Wuhan.

    Bw. Li Wenliang daktari wa macho aliyekuwa na umri wa miaka 35, alifanya kazi katika Hospitali ya Kati ya Wuhan, na alifariki dunia Februari 7 baada ya kuambukizwa nimonia ya COVID-19 Januari 10 akiwa kazini.

    Ripoti hiyo imeitaka Mamlaka ya polisi Wuhan kuangalia upya kutolewa kwa hati ya karipio kwa Bw. Li, hatua ambayo imeamua haifai na kushindwa kufuata taratibu husika za utekelezaji wa sheria, na pia imeitaka polisi kufuta hati hiyo na kuwawajibisha wahusika na kutoa taarifa kwa umma kwa wakati.

    Jana Alhamisi Polisi ya Wuhan imetoa taarifa kupitia ukurasa wake wa Weibo kuhusu uamuzi wa kufuta hati ya karipio kwa daktari Li Wenliang, na kuiomba radhi familia yake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako