• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Cameroon yaendeleza biashara za mipakani licha ya tisgio la corona

    (GMT+08:00) 2020-03-20 19:20:32

    Serikali ya Cameroon imeapa kuendelea na biashara yake na nchi za CEMAC licha ya tishio la ugonjwa hatari wa Covid-19. Mapema wiki hii katika vita dhidi ya Covid-19, Waziri Mkuu wan chi hiyo alitangaza kufungwa kwa "mipaka ya ardhini,angani, na mipaka ya baharini" ya nchi hiyo isipokuwa kwa "ndege za mizigo" na "meli zinazobeba bidhaa muhimu. Kwenye taarifa hiyo hakutoa maelezo zaidi kuhusu magari ya mizigo, hali ambayo imezua wasiwasi mkubwa katika nchi jirani, zinazotegemea biashara hizo kwa maisha yao ya kila siku.

    Hata hivyo jumatano wiki hii, Waziri Mkuu huyo ametangaza kwamba biashara ya mpakani itaendelea hasa na Chad na Jamhuri ya Afrika ya Kati.

    Alhamisi, serikali ya Cameroon tena ilitoa tangazo jipya la kuondoa mtafaruku ikisema Cameroon itaendelea na biashara yake na "nchi zote za CEMAC", ikiwa ni pamoja na Jamhuri ya Afrika ya Kati,Chad, Gabon, Congo na Equatorial Guinea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako