• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wachimbaji wa Tanzanite Tanzania waombwa kuchukua tahadhari dhidi ya corona

    (GMT+08:00) 2020-03-20 19:20:49
    Wachimbaji madini wa Mkoa wa Manyara nchini Tanzania wameombwa kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa corona.

    Wachimbaji hao wametakiwa kufuata maagizo ya serikali ikiwemo kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima na kunawa mikono kila mara kwa hata nje ya migodi yao.

    Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji Madini mkoani humo Justin Nyari alisema wachimbaji hao hawanabudi kuchukua tahadhari ya maambukizi ya ugonjwa huo, kwa kutimiza maagizo ya serikali. Alisema ijapokuwa wachimbaji madini wanavaa vifaa vya barakoa kujikinga na vumbi na hewa chafu wakiwa ndani ya mgodi, lakini kwa sasa wanapaswa kuvaa hata nje ya migodi.

    Aidha alisema tahadhari za afya zinapaswa kuchukuliwa kwa maeneo ya machimbo ukiwamo usafi kwa wachimbaji kunawa mikono kwa maji yanayotiririka na sabuni kwenye maeneo yote migodini na kwenye migahawa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako