• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bei ya Vyakula Rwanda yaongezeka kufuatia Corona

    (GMT+08:00) 2020-03-20 19:21:07

    Bei ya vyakula na bidha muhimu nchini Rwanda zimeendelea kuongezeka kwenye masoko mbalimbali huku sekta ya utalii ikidaiwa kuathirika zaidi. Tayari Rwanda imethibitisha visa 11 vya maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa hatari wa Covid-19 nchini humo.

    Katika kukabiliana na hali hiyo, mamlaka ya nchi hiyo imetangaza hatua kadhaa kukabiliana na kupanda kwa bei kiholela. Benki Kuu ya Rwanda imetangaza kupunguza masharti ya ulipaji wa mikopo ya benki kwa kampuni na watu walioathirika na ugonjwa wa Covid-19.

    Inasemekana kuwa karibu Euro milioni 50 zimetolewa kwa benki za biashara, ambazo zitahitaji ukwasi zaidi. Benki kuu ya Rwanda aidha imesitisha ada ambayo ilikuwa ikitozwa kwa kutoa fedha kupitia mfumo wa kidijitali Ili kuzuia maambukizi ya virusi kupitia biashara ya fedha (kutoa na kupokea fedha).

    Hatua hiyo zinalenga kupunguza athari za Covid-19 kwenye uchumi wa Rwanda. Mojawapo ya sekta zilizoathiriwa zaidi ni sekta ya utalii. Aidha bei imeendelea kupanda kwenye masoko mbalimbali nchini humo, licha ya agizo kutoka Wizara ya Biashara la kutopandisha bei ya bidhaa kama vile mchele, sukari na mahindi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako