Mkuu wa Doria kutoka Idara ya Maendeleo ya Uvuvi, Haji Shomari amesema doria hizo zimerudisha matumaini ya wavuvi kupata kipato kikubwa kufuatia kuwapo kwa hazina ya samaki baada ya eneo la ukanda huo kuingizwa katika orodha mpya ya hifadhi mwaka jana.
Baadhi ya wavuvi wa ukanda wa ghuba ya hifadhi hiyo, walieleza kufurahishwa na doria hizo ambazo lengo lake ni kuzuia uvuvi haramu na kulinda rasilimali za baharini.
Mradi huo uliopewa jina wa Swiofish unatekelezwa chini ya ufadhili wa Benki ya Dunia ukiwa na lengo la kulinda rasilimali za baharini na kuwawezesha wavuvi wadogo kupiga hatua kimaendeleo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |