Uchumi wa Marekani watarajiwa kushuka kwa asilimia 12 katika robo ya pili mwaka huu
Shirika la kimataifa la kutathmini dhamana la Moody nalo limesema, mpango wenye thamani ya dola za kimarekani trilioni 1 utakatolewa na serikali ya Marekani utaongeza shinikizo la madeni la nchi hiyo.
Habari nyingine zinasema, benki kuu ya Marekani ilipanga kununua madeni ya taifa ya dola za kimarekani bilioni75 jana na leo kwa ajili ya kukabiliana na athari ya uchumi inayosababishwa na maambukizi ya virusi vipya vya Corona.
Wizara ya nishati ya Marekani ilitangaza kununua mapipa milioni 30 ya mafuta ghafi yatakayotumika kwa mfuko wa mafuta ya kimkakati ya Marekani ambayo ni pungufu ya mapipa milioni 77 yaliyotangazwa awali.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |