• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mahakama nchini Burundi yamkubalia rais wa zamani kugombea tena nafasi hiyo

    (GMT+08:00) 2020-03-20 19:26:56

    Mahakama ya Katiba nchini Burundi imempitisha rais wa zamani wa nchi hiyo Domitien Ndayizeye, baada ya Tume ya Uchaguzi ya nchi hiyo kukataa ombi lake la kugombea katika uchaguzi huo utakaofanyika Mei 20 mwaka huu.

    Katika kesi iliyosikilizwa jana, uamuzi ulitolewa kuwa Ndayizeye, anayewakilisha muungano wa Kira-Burundi, amekidhi mahitaji ya kugombea nafasi ya urais yaliyowekwa na Tume Huru ya Uchaguzi ya Burundi.

    Machi 10, Tume hiyo ilikataa ombi la Ndayizeye na wagombea wengine watatu kwa kusema hawakukidhi mahitaji yaliyotolewa na katiba ya nchi hiyo ama kanuni za uchaguzi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako