• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UN-Janga la nzige kuwa kubwa zaidi katika pembe ya Afrika

    (GMT+08:00) 2020-03-21 18:03:07

    Wafanyakazi wanaotoa misaada ya kibinadamu wamesema hali ya nzige wa jangwani katika eneo kuu la pembe ya Afrika inatarajiwa kuzidi kuwa mbaya.

    Msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Stephen Dijarric amesema kwa sasa kuna kuzaliana kwa wingi kwa nzige hao, na makundi makubwa yanaanza kujikusanya. Amesema hali hii itahatarisha usalama wa chakula na maisha ya watu, kwa kuwa wimbi lijalo litakuwa kwenye msimu wa kilimo kwenye eneo kubwa la kanda hiyo.

    Kwa sasa kazi ya kunyunyiza dawa kwa ndege ili kuwaua nzige hao inaendelea kwa ushirikiano kati ya serikali na shirika la kilimo na chakula la Umoja wa Mataifa FAO, na tayari hekta elfu kadhaa zimenyunyizwa dawa.

    Kwa sasa madhara ya nzige hao ni makubwa zaidi katika miaka 25 iliyopita kwenye eneo la Afrika Mashariki na Asia Kusini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako