• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kashfa ya wabunge yatikisa jamii ya Marekani

    (GMT+08:00) 2020-03-22 21:30:35

    Kashfa ya mbunge wa seneta wa Marekani kuficha habari kuhusu maambukizi ya virusi vya corona na kuuza hisa kabla ya kuporomoka kwa soko la hisa, imesababisha hasira kubwa katika jamii ya Wamarekani.

    Mbunge huyo Richar Burr ni mwenyekiti wa kamati ya upelelezi na mjumbe wa kamati ya afya katika seneti ya Marekani, yuko kwenye nafasi nzuri ya kupata habari kuhusu hali ya kuenea kwa virusi vya corona kutokana na kwamba anapokea taarifa husika. Na ametumia ipasavyo nafasi hiyo kujinufaisha binafsi.

    Kwa mujibu wa gazeti la New York Times, Burr aliuza hisa alizokuwa nazo Februari 13, ambazo ni wiki kadhaa kabla ya kuporomoka kwa soko la hisa nchini Marekani.

    Zaidi ya hayo alitoa habari husika kwa baadhi ya watu waliofadhili kampeni yake ya uchaguzi Februari 27, ambazo ni siku 13 kabla ya wananchi wa Marekani kupokea taarifa ya serikali ya kutosafiri kwenda Ulaya. Katika kipindi hiki, Burr aliwaambia wamarekani kuwa, kiwango cha hatari ni cha chini sana.

    Lakini Burr sio mwanasiasa pekee wa Marekani aliyetumia maambukizi ya corona kujichotea pesa. Hivi karibuni wabunge wengine watatu wa seneti walifichuliwa kutumia habari walizopata kutokana na nafasi zao, na kuuza hisa kabla ya kuporomoka kwa soko.

    Mbali na hayo, matajiri na watu mashuhuri wanapewa kipaumbele katika suala la kupimwa virusi vya corona. Rais Donald Trump alipoulizwa swali hilo, alijibu huenda hayo ndiyo maisha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako