• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Trump anaswa kwa kubadili "virusi vya corona" kuwa "virusi vya China" katika hotuba yake

    (GMT+08:00) 2020-03-22 21:37:12

    Hivi karibuni, rais Donald Trump wa Marekani aliviita "virusi vya Corona" kwa neno la ubaguzi la "virusi vya China" kwenye mitandao wa kijamii na mikutano na waandishi wa habari, kitendo ambacho vyombo vya habari vimekitaja kama ni nia ya Trump ya kuibebesha China lawama ambayo haistahili wakati idadi ya wagonjwa walioambukizwa virusi vya Corona ikiongezeka.

    Kitendo hicho cha Trump cha kuchafua jina la China kimelaumiwa na jumuia ya kimataifa.

    Hillary Clinton wa Democratic alisema kwenye mtandao wa kijamii kuwa "rais anatoa kauli inayoweza kuchukuliwa kuwa ni ubaguzi wa rangi kwa lengo la kuhamisha ufuatiliaji wa watu juu ya kushindwa kwake katika kushughulikia virusi vya Corona mapema na kwa makini, kutowapima watu wengi, na kutojiandaa vya kutosha katika vita dhidi ya virusi vya Corona.

    Rais Vladimir Putin wa Russia amesema serikali ya China imechukua hatua zenye ufanisi katika kupambana na virusi vya Corona, sio tu imedhibiti maambukizi ya ndani, bali pia imetoa mchango muhimu kwa usalama wa afya wa watu wote duniani. Russia inapongeza sana juhudi hizo za China. China imetoa misaada kwa nchi zinazoathiriwa na virusi hivyo kwa wakati, na kutoa mifano mizuri kwa jamii ya kimataifa. Vitendo vya China ni jibu zuri kwa nchi zinazochochea na kuchafua jina la China.

    Mkuu wa mpango wa dharura wa afya wa Shirika la Afya Duniani WHO Dkt. Michael Ryan amewaambia wanahabari kuwa virusi havijali mipaka, na watu wanaoathiriwa ni wa rangi tofauti na utajiri tofauti, ndio maana ni lazima kuepuka kuhusisha virusi na watu maalum.

    Alipozungumza na wenzake wa Russia, Indonesia, Uholanzi, Singapore na Ufaransa kwa njia ya simu, waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi amesisitiza kuwa China inapinga kithabiti vitendo vyote vya kunyanyapaa juhudi zake za kupambana na virusi na kwamba virusi ni adui wa pamoja wa binadamu, na jamii ya kimataifa inatakiwa kupambana navyo kwa pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako