• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yachangia dola laki 1 za kimarekani kwa WHO kuisaidia Sudan Kusini

    (GMT+08:00) 2020-03-23 09:45:39

    China imetangaza kuchangia dola za kimarekani laki 1 kwa Shirika la afya duniani WHO kwa ajili ya kununua vifaa vya kujikinga na vya matibabu, ikiwa ni sehemu ya msaada kwa Sudan Kusini kwenye mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona.

    Balozi wa China nchini Sudan Kusini Bw. Hua Ning amesema kuzuia na kudhibiti maambukizi kutoka nje imekuwa changamoto kubwa kwa Sudan Kusini. Amesema ugonjwa huo umekuwa janga la dunia na hadi sasa ugonjwa huo umethibtishwa katika nchi zaidi ya 40 barani Afrika. Pia amesema ubalozi huo utashirikiana na Sudan Kusini, WHO na washirika wa kimataifa ili kuzuia maambukizi ya virusi hivyo kwa moyo wa mshikamano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako