• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • CORONA: Rais wa zamani wa Real Madrid Lorenzo Sanz afariki dunia kwa corona

  (GMT+08:00) 2020-03-23 09:48:34

  Rais wa zamani wa timu ya Real Madrid ya Hispania, Lorenzo Sanz amefariki dunia kwa virusi vya corona. Sanz mwenye umri wa miaka 76 alikuwa Rais wa Madrid kwa miaka mitano (1995 - 2000) alifariki Ijumaa wakati akipatiwa matibabu ya virusi vya Corona. Akiwa madarakani 1998 alifanikisha timu yake ya Madrid kucheza fainali ya kwanza ya michuano ya Ulaya baada ya miaka 32. Enzi za uongozi wake akiwa ndani ya Bernabeu timu ya Real Madrid ilishinda Kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya mara mbili. Kabla ya virusi vya corona alikuwa akisumbuliwa na tatizo la upumuaji na figo kabla ya kulazwa kwa siku nane kwa homa kali ya corona na Jumanne hii aliruhusiwa kutoka hospitali.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako