• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Serikali ya Hispania yapanga kurefusha muda wa dharura ya taifa

  (GMT+08:00) 2020-03-23 10:31:35

  Waziri mkuu wa Hispania Bw. Sanchez ametangaza kuwa serikali inapanga kurefusha muda wa dharura ya taifa kwa siku 15.

  Akizungumza kwenye mkutano na wanahabari, Bw. Sanchez amesema kuwa baada ya kusikiliza maoni ya wanasayansi, watapitisha azimio hilo, na kupiga marufuku safari zote zisizo za lazima ndani ya siku 30, lakini marufuku hiyo haiwahusishi raia wa Hispania wanaohitaji kurudi nchini, wakazi wa eneo la Schengen wanaorudi katika makazi yao ya kawaida, watalii wa kigeni wanaorudi katika nchi zao, wafanyakazi wa matibabu, wanadiplomasia na wafanyakazi wa usafirishaji mizigo.

  Aidha Bw. Sanchez ametangaza hatua nyingine kadhaa zinazochukuliwa na serikali, kama wanajeshi kushiriki kusaidia usafirishaji wa wagonjwa na vifaa vya matibabu, kulinda miundombinu muhimu na kutoa rasilimali kwa serikali za mitaa ili kutoa huduma za kusafirisha chakula, vitu vya mahitaji na dawa kwa wazee..

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako