• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yavifuta usajili vyama vya ushirika zaidi ya 3,000 kutokana na usimamizi mbaya

    (GMT+08:00) 2020-03-23 10:31:53

    Waziri wa kilimo wa Tanzania Bw. Japhet Hasunga ametangaza kufuta usajili wa vyama vya ushirika 3,436 kati ya 11,149 nchini kote kutokana na usimamizi mbaya kabla ya tarehe 17 mwezi Aprili.

    Bw. Hasunga amesema hayo kwenye mkutano na wanahabari mjini Dodoma, na kuongeza kuwa ripoti ya ukaguzi wa Shirika la ukaguzi wa usimamizi ya vyama vya ushirika (COASCO) imeonyesha kuwa vyama vingi havikufanya kazi katika maeneo yaliyosajiliwa na vingi havina uongozi.

    Shirika la Kazi Duniani (ILO) linaona vyama vya ushirika ni muhimu katika kuboresha hali ya maisha na kazi kwa watu duniani na kutoa huduma muhimu hata katika maeneo ambayo yamesahaulika kwa serikali na wawekezaji.

    Waziri huyo ameongeza kuwa ripoti ya ukaguzi inaonyesha kuwa hali ya vyama vingi vya ushirika vina usimamizi dhaifu wa kifedha na limbikizo la madeni kutoka kwa wakulima.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako