• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China na Marekani zapaswa kushirikiana kupambana na virusi vya Corona

  (GMT+08:00) 2020-03-23 17:41:41

  Balozi wa China nchini Marekani Bw. Cui Tiankai amesema, China na Marekani zinapaswa kushirikiana katika kupambana na mlipuko wa virusi vya Corona.

  Akihojiwa na kituo cha HBO na mtandao wa AXIOS wa nchini Marekani, Bw. Cui amesema, mlipuko wa COVID-19 ni changamoto ya afya ya umma ya kimataifa, na jamii ya kimataifa inapaswa kushirikiana kwa pamoja kufufua uchumi wa dunia, na kujenga uwezo wa kukabiliana na mlipuko kama huo. Amesema China iko tayari kushirikiana na nchi mbalimblai kutatua changamoto hizo na inapanga kutoa misaada inavyoweza kwa nchi nyingine.

  Bw. Cui pia amesema, ni muhimu kutafuta chanzo cha virusi hivyo, lakini jambo hilo ni juu ya wanasayansi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako