• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya yafunga mpaka wake na Uganda.

  (GMT+08:00) 2020-03-23 18:38:07
  Maafisa katika mpaka kati ya Kenya na Uganda katika Kaunti ya Busia wamefunga Kituo Kikuu cha Mpaka Busia (OSBP) na kupunguza safari za watu kati ya Kenya na Uganda. Hii ni katika juhudi zinazolenga kuimarisha mikakati ya serikali ya kuzuia kusambaa kwa virusi vya corona.

  Hatua hiyo imejiri siku moja tu baada ya Rais wa Uganda Yoweri Museveni kuamrisha kufungwa kwa mipaka yake, saa chache tu baada ya nchi hiyo kutangaza kisa chake cha kwanza cha Covid-19.

  Akitoa taarifa jana kutoka Busia OSBP, Kamishna wa Kaunti Joseph Kanyiri, alisema kufungwa kwa vituo hivyo ni kwa maslahi ya raia wa mataifa hayo mawili.

  Hii ni katika juhudi zinazolenga kuimarisha mikakati ya serikali ya kuzuia kusambaa kwa virusi vya corona.

  Hatua hiyo imejiri siku moja tu baada ya Rais wa Uganda Yoweri Museveni kuamrisha kufungwa kwa mipaka yake, saa chache tu baada ya nchi hiyo kutangaza kisa chake cha kwanza cha Covid-19. Kwa sasa, kupitia majadiliano na kamati za usimamizi wa mipaka katika vituo vya Busia na Malaba, trela zinazosafirisha mizigo katika pande husika zitaruhusiwa kuingia lakini zikiwa na wahudumu wawili pekee.

  Hatua hii imewaathiri maelfu ya wafanyibiashara mpakani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako