• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uganda:  Shirika la ndege la Uganda lasitisha safari zake.

  (GMT+08:00) 2020-03-23 18:39:06

  Shirika la ndege la Uganda limesimamisha safari zote za ndege nchini Uganda ili kukabili tishio la usambazaji wa virusi vya corona. Ikitoa tangazo hilo, usimamizi mkuu wa shirika la ndege la Uganda, limesema kwamba safari zote isipokuwa za mizigo zimefutiliwa mbali kuanzia leo Jumatatu hadi wakati usiojulikana.

  Wasafiri wote walioathirika wameombwa kukatiz asafari zao hadi mamabo yatakapotulia. Haya yanajiri siku mbili baada ya Uganda kutangaza kisa cha kwanza cha corona, ambaye ni mwanaume aliyewasili nchini Uganda akitokea Dubai.

  Ni hatua ambayo pia imechukuliwa na serikali ya Kenya. Hapo jana, waziri wa Afya Mutahi Kagwe alitangaza kwamba Kenya haitaruhusu safari zozote za ndege kuanzia siku ya Jumatano wiki hii.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako