• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Pato la uchumi la bara la Afriika (GDP) laathirika.

    (GMT+08:00) 2020-03-23 18:39:29
    Mataifa ya Afrika yamepoteza takriban dola bilioni 29 kwa kipindi cha miezi mitatu kutokana na virusi vya corona.

    Ripoti maalum ya kamati ya Umoja wa Mataifa kuhusu Uchumi barani Afrika inakadiria kwamba virusi hivi vya corona huenda vikapunguza pato la uchumi la bara la Afrika kwa asilimia 1.4, kati ya dola trilioni 2.1. Hii inatokana na kusambaa sana kwa virusi hivi ambavyo vimeathiri biashara kote barani Afrika.

    Ripoti hiyo pia inasema kwamba ukuahi wa uchumi kwa mwaka barani Afrika utashuka chini kutoka asilimia 3.2 mwezi Februari hadi asilimia 1.8 mwezi huu wa Machi. Ripoti hiyo ikitoa onyo kwamba hali itakuwa mbaya zaidi kwani mataifa mengi yanazidi kushuhudia ongezeko la visa vya wale waliombukizwa viruzi vya corona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako