• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viwanda vya pombe nchini Uganda vyageukia utengenezaji wa visafisha mikono kupambana na COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-03-23 19:19:53

    Viwanda vya kutengeneza pombe nchini Uganda vimegeukia utengenezaji wa visafisha mikono wakati nchi hiyo ikiongeza juhudi katika kupambana na kuenea kwa virusi vya Corona.

    Waziri wa nchi anayeshughulikia uwekezaji nchini humo Bi. Evelyn Anite amesema kuwa, watengenezaji hao, wamekubali kukabiliana na uhaba wa visafisha mikono nchini humo.

    Amesema watengenezaji hao watatumia lita milioni 7.3 za pombe walizo nazo kwenye viwanda vyao kutengeneza visafisha mikono vya gharama nafuu na vyenye ubora wa juu. Ameongeza kuwa, serikali itawaunga mkono wazalishaji hao kupitia kuondoa kodi ya nyongeza ya thamani na ushuru ili kuwasaidia kuongeza uzalishaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako