China imeikosoa Marekani kwa kuinyanyapaa na kuibebesha lawama za kushindwa kupambana na virusi vya corona, na kusema kitendo hicho si cha kimaadili na hakitaisaidia Marekani kufanya vizuri kazi zake wala hakisaidii ushirikiano wa kimataifa katika mapambano dhidi ya virusi hivyo.
Kauli hiyo imekuja baada ya habari kuwa Baraza la Usalama wa Taifa nchini Marekani limezitaka idara mbalimbali za nchi hiyo kuratibu kauli zao kwa kuiambia dunia kuwa virusi hivyo vinaenea duniani kutokana na China kuficha habari. Akizungumzia hilo, Geng amesema tangu maambukizi ya virusi vya corona yalipuke, China imefuata kanuni za uwazi na uwajibikaji na kutoa taarifa kwa Shirika la Afya Duniani WHO na nchi na sehemu mbalimbali ikiwemo Marekani. Katika miezi miwili iliyopita, wachina wamejitahidi kupambana na virusi hivyo na kuzipa nchi nyingine muda wa kujiandaa. Lakini serikali ya Marekani haikutumia muda huo muhimu, na kwamba siku 50 zimepita tangu itangaze wazuia wageni waliotoka China ndani ya siku 14 kuingia nchini humo, lakini kesi zilizothibitishwa nchini humo zimeongezeka kutoka kumi tu ya wakati ule, hadi elfu 30 ya leo.
Geng ameitaka Marekani iache kufanya maambuziki hayo kuwa ya kisiasa, iache kuchafua sura za China na nchi nyingine, na badala yake kujizatiti zaidi kwenye juhudi za kupambana na virusi vya corona na kushirikiana na nchi nyingine kuchangia usalama wa afya ya umma duniani.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |