• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Katibu mkuu wa UN atoa wito wa kusimamisha vita kote duniani ili kupambana na virusi vya Corona

  (GMT+08:00) 2020-03-24 10:05:24

  Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres ametoa wito wa kusimamisha vita kote duniani ili kupambana na virusi vya Corona.

  Bw Guterres amezihimiza pande zote zisitishe mapambano na kutilia maanani kupambana na virusi vya Corona, na kusema hatua hiyo itaweka mazingira mazuri ya kuwaokoa wagonjwa na kufikisha huduma za matibabu kwenye sehemu zisizo na uwezo wa kupambana na virusi hivyo.

  Amesema virusi vya Corona ni adui wa pamoja wa binadamu wote, na hali ya matibabu kwenye sehemu zenye vita imekuwa mbaya zaidi, kama madaktari wachache wa huko wakiathiriwa na virusi, wakimbizi watakumbwa na tatizo kubwa zaidi. Pia anataka kuweka mipango ya mfululizo ili kukabiliana na athari mbaya za kiuchumi na kijamii zinazotokana na mlipuko wa virusi hivyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako