• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Benki kuu ya Kenya yashusha riba ya mikopo ili kupambana na COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-03-24 10:07:02

    Benki kuu ya Kenya jana jumatatu imeshusha kiwango cha riba ya mikopo kutoka asilimia 8.25 hadi kufikia asilimia 7.25 ili kukabiliana na mlipuko wa virusi vya corona.

    Mkurugenzi wa Benki hiyo Petrick Njoroge ambaye aliongoza mkutano wa Kamati ya Sera za Fedha MPC uliofanyika Nairobi, amesema hatua hiyo ya kisera inalenga kuzuia msukosuko wa afya unaotokana na virusi vya Corona usibadilike kuwa msukosuko mkubwa wa kiuchumi na kifedha. Ameongeza kuwa Kamati inafuatilia kwa karibu athari za mabadiliko hayo ya kisera, na iko tayari kuchukua hatua zaidi kulingana na maendeleo ya uchumi wa dunia.

    Bw. Njoroge amesema kutokana na mlipuko wa virusi vya Corona, ukuaji wa uchumi wa Kenya unatarajiwa kupungua kwa kiasi kikubwa mwaka 2020, kutoka asilimia 6.2 iliyokadiriwa hadi kufikia asilimia 3.4.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako