• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yapanga kuchukua hatua kuwasaidia wafanyakazi wa sekta isiyo rasmi wakati wa mlipuko wa COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-03-24 10:07:18

    Kenya inapanga kuchukua hatua za kuchochea uchumi ambazo zitawakinga wafanyakazi wa sekta isiyo rasmi dhidi ya athari za mlipuko wa COVID-19.

    Waziri wa leba Bw Simon Chelugui amewaambia wanahabari mjini Nairobi kuwa makundi maalumu ya watu yameathiriwa zaidi na vizuizi vya usafiri ambavyo vimewekwa na serikali za nchi mbalimbali kote duniani, na watatoa mapendekezo kwa Hazina ya Taifa kuhusu hatua zitakazochukuliwa kwenye sekta ya leba ambazo zimesanifiwa kuwakinga wafanyakazi, hasa wale walio kwenye sekta isiyo rasmi dhidi ya athari za kupungua kwa uchumi kutokana na mlipuko wa virusi vya corona.

    Kenya iliripoti maambukizi ya kwanza ya virusi vya corona Machi 13, na serikali ikaamua kufunga shule, kupiga marufuku mikusanyiko ya watu na kuwataka watu kukaa nyumbani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako