• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanasiasa wa Afrika wasisitiza kuwa dunia nzima inatakiwa kushirikiana kupambana na virusi vya Corona

    (GMT+08:00) 2020-03-24 10:47:39

    Hivi karibuni wanasiasa wa nchi nyingi za Afrika walipohojiwa na Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG wamesema hatua zenye ufanisi za China zimefanikiwa kuzuia kuenea kwa virusi vya Corona. Sasa linalotakiwa kufanywa ni kushirikiana katika kupambana na ugonjwa huo, badala ya kulaani au kupaka matope jina. Waziri wa Afya wa Ethiopia Bibi Lia Tadesse amesema virusi vya Corona ni changamoto inayoikabili dunia nzima.

    "Virusi hivyo vinawashambulia binadamu wote bila kutofautisha makabila, tamaduni, rangi za ngozi au dini. Ndiyo maana havipaswi kuhusishwa na kundi la watu, rangi ya ngozi au kabila. Jumuiya ya kimataifa inatakiwa kukabiliana kwa pamoja ugonjwa huo, badala ya kuuhusisha na nchi au kabila. Tunalotakiwa kufanya ni kushirikiana kupambana na ugonjwa huu ili kushinda vita dhidi ya virusi hivyo."

    Mkurugenzi wa Kituo cha Udhibiti wa Magonjwa cha Afrika Bw. John Nkengasong amesema, mapambano dhidi ya ugonjwa huo yanategemea ushirikiano wa kimataifa, badala ya kupaka matope jina au kubagua sehemu fulani. Anasema:

    "Naona kuwa haya ni mapambano ya dunia nzima, ambayo yanahitaji mshikamano na ushirikiano wa dunia nzima, sio kupaka matope jina la Asia au kuwabagua watu walioambukiwza ugonjwa huo. Adui yetu ni virusi, wala si Afrika, Ulaya au bara la Amerika. Tunachotakiwa kufanya ni kupambana na adui yetu halisi---virusi vya Corona."

    Balozi wa Djibouti kwenye Umoja wa Afrika Bw. Mohammed Idris Farah amepongeza juhudi za China katika kupambana na ugonjwa huo, akiona kuwa uzoefu wa China unatakiwa kuigwa.

    "Mapambano ya Afrika dhidi ya virusi vya Corona yanahitaji kuiga uzoefu wa China. China ilichukua hatua madhubuti katika kuzuia kuenea kwa virusi hivyo, ni lazima Afrika ichukue hatua kama hizo. Afrika haina fedha za kupambana na ugonjwa huo kwa muda mrefu, hivyo inahitaji kushirikiana na wenzi ikiwemo China kupambana na ugonjwa huu."

    Shirika la ndege la Ethiopia ambalo ni shirika kubwa zaidi la ndege barani Afrika, lilisafirisha misaada ya vifaa kutoka China kwenda Addis Ababa. Mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo Bw. Tewolde Gebremariam anasema:

    "Ni hali mbaya sana kwamba virusi vya Corona vinaenea dunia nzima. Ndiyo maana ni lazima tufanye juhudi kwa pamoja kujilinda. Endapo tutalaumiana tutapunguza ufuatiliaji juu ya ugonjwa huu. Waziri mkuu wa nchi yetu na Bw. Jack Ma wameanzisha kampeni ya uchangishaji fedha. Sasa tunashughulikia usafirishaji wa vifaa, ili kuwahakikisha watu wanalindwa. Lakini kitendo cha kupaka matope jina la nchi nyingine hakisaidii kitu."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako