• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais Xi Jinping wa China afanya mazungumzo kwa njia ya simu na marais wa Ufaransa na Misri

  (GMT+08:00) 2020-03-24 10:48:09

  Rais Xi Jinping wa China jana usiku alifanya mazungumzo kwa njia ya simu na rais Emmanuel Macron wa Ufaransa. Rais Xi amejulisha hali ya kinga na udhibiti wa maambukizi ya virusi vya corona, pia amesisitiza kuwa China na Ufaransa zinabeba majukumu ya kulinda usalama wa afya ya umma wa kikanda na kimataifa, na zinapaswa kufanya ushirikiano, kuhimiza miradi ya utafiti ya pamoja, kuunga mkono kazi ya Shirika la afya duniani (WHO), na kuzisaidia kwa pamoja nchi za Afrika katika kuzuia na kudhibiti maambukizi ya virusi hivyo.

  Rais Macron ameishukuru China kwa msaada wake, na kusema Ufaransa inapenda kufanya ushirikiano wa afya na China, kupambana na mlipuko wa virusi vya corona, na kukabiliana kwa pamoja na athari zake kwa uchumi wa dunia.

  Siku hiyo usiku rais Xi pia alifanya mazungumzo kwa njia ya simu na rais Abdel Fattah al Sisi wa Misri. Rais Xi amesema China inapenda kubadilishana na Misri habari kuhusu virusi, uzoefu wa kinga na tiba na matokeo ya utafiti, na pia inapenda kutoa vifaa vya matibabu kwa Misri na kuunga mkono kazi ya kuzuia na kudhibiti maambukizi ya virusi nchini Misri.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako