• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Falling Waters yajiandalia fainali za Chapa Dimba

    (GMT+08:00) 2020-03-24 15:59:41

    Kocha wa timu ya wasichana ya Falling Waters, Emman 'Gullit' Wambuchi amesema wanapania kujituma vikali katika fainali za kitaifa kupigania taji la Chapa Dimba na Safaricom Season Three nchini Kenya. Falling waters awali ikifahamika kama Barcelona Ladies kwa mara nyingine itawakilisha Mkoa wa Kati katika fainali hizo. Kwenye mashindano ya kitaifa msimu uliopita warembo hao walitolewa katika nusu fainali na Kitale Queens iliyoibuka malkia. Vigoli hao chini ya nahodha, Miriam Lutomia walibeba taji la eneo hilo walipoteremsha soka safi na kuwafunga Limuru Starlets kwa magoli 3-1.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako