• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: PSG, Real Madrid na Manchester City zaingia vitabi kumng'oa Skriniar Inter Milan

  (GMT+08:00) 2020-03-24 16:02:49

  Beki kisiki wa Inter Milan, Milan Skriniar amewaingiza vitani vigogo wa klabu za Paris Saint-German (PSG), Real Madrid na Machester City ambao wanapishana jijini Milan kusaka saini yake kwa ajili ya dirisha kubwa lijalo la usajili. Skriniar ambaye ni raia wa Slovakia, amekuwa katika kiwango bora zaidi msimu huu na katika dirisha dogo la usajili la mwezi Januari alikaribia kutimkia Barcelona katika dakika za mwisho, lakini klabu hizo mbili zilishindwa kufikia makubaliano ya malipo ya ada. Kwa sasa mchezaji huyo ana thamani ya Pound milioni 85 sokoni.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako