• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mji wa New York umekuwa mji ulioathiriwa zaidi na virusi vya Corona ukiwa na wagonjwa zaidi ya elfu 13

  (GMT+08:00) 2020-03-24 17:39:26

  Takwimu zilizotolewa na Kituo cha Mifumo ya Sayansi na Uhandisi katika Chuo Kikuu cha John Hopkins zimeonyesha kuwa, idadi ya kesi zilizothibitishwa kuwa maambukizi ya virusi vya Corona katika Mji wa New York nchini Marekani imefikia 13,119 mpaka kufikia jana usiku kwa saa za huko, huku watu waliofariki kutokana na maambukizi hao wakifikia 124.

  Mji huo wenye idadi ya watu milioni 8.6 umekuwa chanzo kipya cha mlipuko huo, ukichukua karibu asilimia 30 ya idadi ya jumla ya maambukizi nchini Marekani, ambayo imefikia 43,901.

  Meya wa New York Bill de Blasio amesema kuwa hali katika mji huo inaweza kuwa mbaya zaidi, na kuongeza kuwa ni mwanzo wa kitu ambacho kitakuwa kibaya zaidi katika miezi miwili ijayo. Amewataka wakazi wa mji huo kubadili mwenendo wa maisha yao, na kwamba wanahitaji msaada kutoka serikali kuu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako