• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Marekani zapaswa kushirikiana katika mapambano dhidi ya COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-03-24 19:53:42

    Baada ya virusi vya Corona kuendelea kuenea, watu zaidi laki 3 wameambukizwa kote duniani. Lakini wakati nchi mbalimbali duniani zinashirikiana kupambana na virusi hiyo, serikali ya Marekani inatumia nguvu yake katika kulaumu China.

    Tovuti ya The Daily Beast imeinukuu taarifa ya ikulu ya Marekani inayosema, serikali ya nchi hiyo inawataka maofisa watumie kauli moja ya kulaumu China kuficha taarifa za kweli kuhusu maambukizi ya virusi vya Corona na kusababisha kuenea kwa virusi hivyo dunia nzima. Mkurugenzi wa kituo cha utafiti kuhusu Marekani cha Chuo Kikuu cha Beijing Bw. Wang Yong amesema, zikiwa nchi kubwa zaidi za kiuchumi duniani, ushirikiano kati ya China na Marekani katika mapambano dhidi ya virusi vya Corona ni muhimu sana kwa Marekani na hata dunia. Mashambulizi ya maneno kutoka kwa serikali ya Marekani kuhusu China yanaweza kuharibu uhusiano na kuzuia mawasiliano kati ya nchi hizo mbili.

    Lawama za serikali ya Marekani dhidi ya China hazina msingi wowote, kwani baada ya maambukizi ya virusi vya Corona kutokea, China ilitangaza taarifa kuhusu maambukizi hayo kwa wazi na haraka, na kuchukua hatua mbalimbali za kuzuia maambukizi. China pia imetuma madaktari na kutoa msaada wa vifaa kwa Italia, Iran na nchi nyingine zinazokumbwa zaidi na maambukizi hayo. Hivi karibuni jamii ya kimataifa imepinga kithabiti kitendo cha rais wa Marekani Donald Trump na waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Mike Pompeo kuita virusi vya Corona kuwa virusi vya China. Hata kituo cha kinga na udhibiti wa magonjwa cha Marekani nacho kimepinga kauli hiyo na kusema italeta ubaguzi kwa wachina na watu wote wa Asia. Lakini kwa nini serikali ya Marekani inashikilia kufanya hivyo?

    Wachambuzi wanaona kuwa, kitendo hiki cha rais Trump kina sababu mbili, kwanza ni kujaribu kuondoa wajibu wake, na kuwafanya wananchi wake kutoilaumu serikali kwa kutochukua hatua za kutosha za kupambana na maambukizi, pili ni kuendelea kuchafua na kudharau China ambayo ni mpinzani wake mwenye nguvu.

    Gazeti la Washington Post nalo linasema kuwa idara za upelelezi za Marekani zimetoa onyo kuhusu maambukizi hayo mapema mwezi Januari, lakini rais Trump na bunge la Marekani hazikutilia maanani, na kutochukua hatua mara moja kuzuia maambukizi hayo.

    Hadi saa 12 jioni jana, Marekani imetangaza maambukizi 43,214, na vifo 533 kutokana na virusi vya Corona. Masuala mbalimbali yameonekana katika jamii ya Marekani, shule zimefungwa, baadhi ya familia zenye matatizo ya kiuchumi zinakabiliwa na upungufu wa chakula, sekta ya huduma imeathiriwa, idadi ya watu wasio na ajira imeongezeka, pia kuna uhaba mkubwa wa vifaa vya kinga ya matibabu.

    Kutokana na ukweli huo, serikali ya Marekani inashindwa kufafanua sababu za kutofanya juhudi zote katika kinga na udhibiti wa ugonjwa huo, na hivyo kuilaumu China ni njia rahisi zaidi. Mwanachama wa chama cha demokrasia cha Marekani Hillary Clinton amesema, rais Trump anajaribu kusambaza kauli ya ubaguzi ili kuficha kosa la serikali yake katika mapambano dhidi ya virusi vya Corona.

    Bw. Wang Yong anaona kuwa, sababu kubwa ya kitendo hiki cha rais Trump ni kwa ajili ya kupambana na Chama cha Demokrasia na kupata ushindi katika uchaguzi.

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. António Guterres amesema, maambukizi ya virusi vya Corona ni changamoto kwa binadamu ambao unahitaji mshikamano. Kukabiliana na changamoto hiyo kubwa, upande mmoja pekee utashindwa, ushirikiano ndio njia sahihi ya kupata ushindi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako