• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China kuadhibu vikali vitendo vinavyokiuka sheria za ukaguzi wa afya katika forodha

  (GMT+08:00) 2020-03-24 20:06:40

  Kutokana na hali mbaya ya kuenea kwa virusi vya Corona duniani, China imetoa kipaumbele katika kukinga maambukizi ya nje katika kukabiliana na ugonjwa huo. Hivi karibuni mahakama kuu, idara kuu ya uendeshaji wa mashtaka, wizara ya usalama wa umma, wizara ya sheria na idara kuu ya forodha nchini China zimetoa kwa pamoja mapendekezo kuhusu uhalifu dhidi ya ukaguzi wa afya katika vituo vya forodha.

  Mapendekezo yaliyotolewa tarehe 16 mwezi huu na idara hizo yameeleza aina sita za vitendo vinavyokiuka sheria za ukaguzi wa afya katika vituo vya forodha, ikiwemo kukataa ukaguzi huo, kutojaza fomu kuhusu afya kutokana na hali halisi, na kutoa hati bandia au kusahihisha hati. Kama vitendo hivyo vikisababisha kuenea kwa magonjwa ya kuambukiza, vitaadhibiwa kisheria. Mkurugenzi wa ofisi ya utafiti ya mahakama kuu ya China Jiang Qibo anasema,

  "Bila kujali ni raia wa China au wageni, au mtu asiye na uraia, akifanya uhalifu dhidi ya ukaguzi wa afya anapoingia nchini China, atafikishwa mbele ya sheria zetu."

  Kwa mujibu wa sheria za kijinai za China, uhalifu wa kukwepa ukaguzi wa afya katika forodha na uhalifu wa kuvuruga juhudi za kukabiliana na magonjwa ya kuambukiza vyote viko chini ya aina ya uhalifu wa kuvuruga utaratibu wa usimamizi wa jamii, tofauti ni kwamba uhalifu wa kuzuia juhudi za kukabiliana na magonjwa ya kuambukiza unahusika na magonjwa yote makuu ya maambukizi, na uhalifu wa kukwepa ukaguzi wa afya katika forodha unahusika na magonjwa ya Tauni, Kipindupindu, homa ya manjano na magonjwa mengine yanayotangazwa na Baraza la Serikali la China.

  Mkurugenzi wa ofisi ya utafiti wa sera za sheria ya idara kuu ya Mwendesha mashtaka ya China Gao Jingfeng amesema, watu wanaovuruga juhudi za kukabiliana na COVID-19 wanapoingia China, wanaweza kukutwa na kosa la uhalifu wa kuvuruga ukaguzi wa afya katika forodha pamoja na uhalifu wa kuzuia juhudi za kukabiliana na magonjwa ya kuambukiza. Anasema,

  "Licha ya kukataa ukaguzi wa afya forodhani, mtu fulani akikataa tena hatua za kukabiliana na maambukizi ya magonjwa baada ya kuingia nchini China, atakutwa na kosa la uhalifu wa kukwepa ukaguzi wa afya katika forodha pamoja na uhalifu wa kuzuia juhudi za kukabiliana na magonjwa ya kuambukiza, na kuadhibiwa kufuatia sheria kali zaidi."

  Gao amesisitiza kuwa, kitendo cha kukwepa ukaguzi wa afya katika forodha kinachosababisha mambukizi ya virusi vya Corona au hatari kubwa ya maambukizi hayo kitachukuliwa kuwa ni uhalifu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako