• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • CORONA: Bilionea Evangelos Marikanis na nyota wa Chelsea Callum Hudson-Odoi wapona Corona

  (GMT+08:00) 2020-03-25 08:56:03

  Mmiliki wa klabu ya Nottingham Forest na Olympiacos Evangelos Marikanis, 52, aliyetangaza kuwa na maambukizi ya virusi vya corona siku kadhaa nyuma methibitisha kuwa amepona virusi hivyo na yupo sawa kuendelea na mfumo wa maisha yake ya kawaida. Evangelos Marikanis alitangaza kuwa na maambukizi na baadaye kukaa karantini kwa siku 14. Bilionea Marikanis anamiliki miradi mbalimbali kama timu ya Olympiacos ya nchini kwao Ugiriki na Nottingham Forest ya England lakini pia ni mmiliki wa meli kadhaa. Naye nyota wa Chelsea Callum Hudson-Odoi apona corona na kurejea katika maisha yake ya kawaida baada ya kutengwa wiki kadhaa nyuma Kwa kugundulika kuwa na maambukizi. Odoi alikuwa staa wa kwanza wa soka England kugundulika kuwa ana maambukizi ya virusi vya corona, kwa sasa Odoi ameanza kufanya mazoezi binafsi baada ya kupona na kuendelea na maisha yake ya kawaida. Odoi alijitangaza kupata maambukizi hayo lakini alieleza kuwa anafuata taratibu za wataalam wa afya kama zinavyotaka, Ligi Kuu England ikiwa imesimama hadi April 30 2020 Odoi anaendelea na mazoezi binafsi ya kujiweka fiti akiwa nyumbani kwake.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako