• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Griezmann apewa mbinu za kuimarisha soka yake ndani ya Barcelona

  (GMT+08:00) 2020-03-25 08:56:21

  Nyota wa zamani wa Barcelona, Rivaldo amefunguka kuwa uwepo wa mchezaji Antonie Griezmann ndani ya klabu hiyo umemkumbusha uwepo wa Coutinho. Rivaldo amemfananisha Griezmann katika msimu wake wa kwanza ndani ya Barca kama ambavyo ilikuwa kwa Coutinho. Griezmann amekuwa akipambana katika msimu wake huu wa kwanza ndani ya Barca lakini bado inaonekana mambo hayajamnyookea. Rivaldo anaona Griezmann anatakiwa kuonyesha kitu tofauti kwani Messi hana muda mrefu ndani ya klabu hiyo, na kusisitiza kuwa Barcelona ilimsajili kutokana na ubora wake hivyo anatakiwa kuonyesha utofauti. Griezmann alijiunga Barcelona akitokea Atletico Madrid kwa kiasi cha euro milioni 120, lakini bado hajaonyesha cheche zake ndani ya kikosi hicho. Msimu huu katika michuano yote Griezmann amefunga jumla ya mabao 13 tu na kati ya hayo manane amefunga kwenye La Liga.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako