• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasisitiza tena kushirikiana na Ethiopia kwenye mapambano dhidi ya virusi vya Corona

    (GMT+08:00) 2020-03-25 09:55:09

    Ubalozi wa China nchini Ethiopia umesema serikali na wananchi wa China wataendelea kushirikiana na nchi za Afrika kwenye mapambano dhidi ya virusi vya Corona.

    Kwenye taarifa hiyo China imezishukuru Ethiopia na nchi nyingine za Afrika kwa kuiunga mkono China hapo awali wakati wa mlipuko wa virusi vya Corona.

    Taarifa hiyo pia imesema siku zote China inaziunga mkono nchi za Afrika kadri iwezavyo kwa njia tofauti ili kupambana na virusi vya Corona. Wataalamu wa China pia wametoa mafunzo kwa wafanyakazi wa Shirika la ndege la Ethiopia kwa ajili ya kuongeza uwezo wao wa kujikinga dhidi ya virusi. Shirikisho la biashara kati ya China na Afrika limeipatia Ethiopia vitendanishi na vifaa vya upimaji vyenye thamani ya dola elfu 22 za kimarekani.

    Tarehe 22 mwezi huu vifaa kutoka kwa mfuko wa Jack Ma wa China kwa ajili ya nchi 54 za Afrika katika kupambana na virusi vya Corona vilifika Ethiopia. Waziri wa afya wa Ethiopia Dk. Lia Tadesse amesema Ethiopia inashirikiana kwa karibu na China na kuiga uzoefu wa China katika kupambana na virusi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako