• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mkuu wa UM alitaka kundi la G20 kuchukua uongozi katika mapambano dhidi ya COVID-19

  (GMT+08:00) 2020-03-25 10:25:31

  Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amelitaka kundi la nchi 20 (G20) ambalo ni kundi kubwa zaidi la kiuchumi duniani, kuchukua uongozi katika mapambano dhidi ya mlipuko wa virusi vya Corona duniani.

  Bw. Guterres amewataka viongozi hao waratibu hatua zao katika kupambana na virusi hivyo, kupunguza athari za kijamii na kiuchumi zinazoletwa na janga hili, na kuhakikisha kuwa uchumi wa dunia unafufuka kwa njia shirikishi na ya kudumu. Amesema viongozi wa kundi la G20 watakuwa na fursa ya kukabiliana na matishio mbalimbali ya COVID-19 kwa hatua madhubuti, hali ambayo itaonesha mshikamano na watu wa dunia nzima, haswa wale walioko hatarini zaidi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako