• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Hisa za Kenya zashuka kwenye kiwango cha chini zaidi kutokana na hofu ya kuenea kwa virusi vya Corona

  (GMT+08:00) 2020-03-25 10:27:43

  Vielezo vya soko la hisa la Nairobi NSE vinaonesha kuwa soko hilo limeshuka na kuwa katika kiwango cha chini katika miaka 20 iliyopita.

  Takwimu za NSE zimeonesha kuwa, vielelezo vyake ambavyo vinapima hali ya hisa ya Afrika Mashariki, vimepoteza alama 71.38 na kufikia 1,887.17.

  Wachambuzi wanaona kuwa, hii ni hali mbaya zaidi kulikabili soko la hisa la Kenya, na kwamba inatokana na hofu inayoletwa na maambukizi ya virusi vya Corona, inayowafanya wawekezaji wengi wa kigeni kuuza hisa zao na kuondoka sokoni. Hadi sasa wagonjwa 25 wameripotiwa kuambukizwa virusi vya Corona nchini Kenya.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako