• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Trump aitaka Marekani ifungue tena uchumi wake ndani ya wiki tatu licha ya hofu ya kushindwa kudhibiti COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-03-25 10:28:09

    Rais Donald Trump wa Marekani amesema anaitaka Marekani "ifunguliwe tena" kabla ya sikukuu ya Pasaka inayoangukia Aprili 12 mwaka huu, licha ya onyo kuwa kufanya hivyo kutaleta hatari kubwa kwa juhudi za kudhibiti mlipuko wa virusi vya Corona nchini humo. Kauli hiyo imekuja kufuatia majimbo 17 ya nchi hiyo kutoa amri kwa wakazi kukaa nyumbani kuanzia leo Jumatano.

    Rais Trump amesema serikali yake itatathmini upya maagizo ya kuepuka mikusanyiko kwa siku 15, yanayolenga kupunguza kasi ya kuenea kwa virusi, akipendekeza kufuta maagizo hayo mapema wiki ijayo.

    Akizungumzia uchumi wa Marekani, rais Trump amesema "Wakikifungua tena nchi mapema zaidi, ukuaji wa uchumi utakuwa bora zaidi".

    Hadi kufikia jumatatu Marekani ilikuwa imeripoti maambukizi zaidi ya elfu 53 ya virusi vya Corona, ambayo yamesababisha vifo vya watu 696.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako