• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Sudan Kusini na Zimbabwe zapata vifaa vya matibabu kutoka Mfuko wa Jack Ma

  (GMT+08:00) 2020-03-25 10:29:17

  Sudan Kusini imepata vifaa vya matibabu kutoka kwenye Mfuko wa Jack Ma na Mfuko wa Alibaba, ambavyo ni pamoja na mask laki moja, vitendanishi elfu 20 vya upimaji na nguo za kujikinga elfu moja.

  Naibu waziri wa mambo ya nje wa Sudan Kusini Bw. Deng Dau Deng amesema, mchango huo umefika kwa wakati unaofaa wakati Sudan Kusini inapofanya juhudi kuzuia virusi vya Corona visiingie nchini humo.

  Zimbabwe pia jana ilipokea vifaa vya matibabu vilivyochangiwa na Mfuko wa Jack Ma kupitia Umoja wa Afrika, ambavyo ni pamoja na vitendanishi elfu 20, mask laki moja na nguo za kujikinga elfu moja.

  Taarifa iliyotolewa na wizara ya afya ya Zimbabwe imesema, wizara hiyo inaushukuru Mfuko wa Jack Ma kwa msaada wake, na inafanya juhudi kuhakikisha usambazaji wa vifaa hivyo, ili viweze kufika kwa wenye mahitaji zaidi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako