• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais Xi Jinping afanya mazungumzo kwa njia ya simu na marais wa Brazil, Poland na Kazakhstan

  (GMT+08:00) 2020-03-25 10:29:54

  Rais Xi Jinping wa China jana usiku kwa nyakati tofauti amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na rais Jair Bolsonaro wa Brazil, rais Andrzej Duda wa Poland, na rais Kassym-Jomart Tokayev wa Kazakhstan, na kutoa salamu za dhati na uungaji mkono kwa serikali na watu wa nchi hizo tatu katika kupambana na virusi vya Corona.

  Rais Xi amesema hivi karibuni, janga hilo limeenea kwa haraka katika sehemu nyingi duniani, hivyo ni muhimu kwa nchi zote kuimarisha ushirikiano, na kila wakati China inashikilia wazo la jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja, kutoa uzoefu wa kuzuia, kudhibiti, na kutibu ugonjwa wa COVID-19 kwa Shirika la WHO na jamii ya kimataifa.

  Rais Xi ameongeza kuwa China inapenda kutoa misaada kwa nchi hizo tatu ili kuzuia kuenea kwa virusi vya Corona, na kulinda kwa pamoja usalama wa afya ya umma.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako