• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yaimarisha kwa pande zote hatua za kutuliza ajira zinazokabiliana na maambukizi ya virusi vya Corona

  (GMT+08:00) 2020-03-25 18:29:01

  Baraza la Serikali la China limesema, ili kukabiliana na athari ya maambukizi ya virusi vya Corona, China imetekeleza hatua za kinga na udhibiti kwa usahihi, kuharakisha makampuni kuanza tena uzalishaji, kuwaongoza wafanyakazi vibarua kupata ajira kwa usalama na utaratibu, pia kuongeza nafasi za ajira kwa wahitimu wa vyuo vikuu, ili kuhakikisha utulivu wa jumla wa ajira.

  Kutokana na maambukizi ya virusi vya Corona, baadhi ya kampuni zinakabiliana na matatizo katika uzalishaji na uendeshaji, hivyo shinikizo la utulivu wa ajira linaongezeka. Tarehe 18 Machi, Baraza la Serikali la China lilitoa pendekezo la utekelezaji wa hatua za kutuliza ajira kutokana na maambukizi ya virusi vya Corona. Naibu waziri wa Nguvukazi na Usalama wa Jamii Bw. You Jun amesema, sehemu mbalimbali nchini zinatakiwa kutoa sera za kupunguza ushuru na ada, pendekezo hilo limezitaka sera hizo zitekelezwe kwa haraka ili kutoa nishati kwa kampuni hasa ndogo na za kati na kufanya juhudi zote kutuliza ajira.

  "Takwimu zinaonyesha kuwa, katika mwezi Februari kampuni zimepunguza ada za bima ya uzee, ukosefu wa ajira na majeraha kazini kwa jumla ya yuan bilioni 123.9, na huenda ada hizo zitapunguzwa kwa zaidi ya bilioni 500 kati ya mwezi Februari hadi Juni, na idadi halisi inaweza kuzidi makadirio ya awali. Licha ya kurudisha ada za bima ya ukosefu wa ajira kwa kampuni ndogo na zenye ukubwa wa kati, kwa zile kampuni zisizopunguza wafanyakazi ama kupungua wafanyakazi wachache, kigezo cha kurudisha ada ya bima ya ukosefu wa ajira kitaongezeka kuwa asilimia 100 kutoka asilimia 50 ya ada zilizotolewa mwaka uliopita. Kampuni zote za Hubei zitanufaika. "

  Bw. You Jun amefahamisha kuwa, kwa sasa idadi ya wafanyakazi vibarua imefikia milioni 290, na milioni 170 kati yao wanafanya kazi nje ya maskani zao. Pendekezo hilo linahakikisha kuwaelekeza wafanyakazi vibarua kupata ajira kwa usalama na utaratibu, kuwahamasisha kupata ajira katika sehemu za karibu, kutoa kipaumbele kwa wafanyakazi vibarua wenye matatizo ya kiuchumi, na kuwasaidia wafanyakazi vibarua kupata ajira na kuongeza mapato.

  Bw. You Jun pia amesema, idadi ya wahitimu wa vyuo vikuu vya China itafikia milioni 8.74, ambayo ni ya juu zaidi katika historia. Ili kupanua nafasi za ajira kwao, pendekezo hilo limehakikisha kwamba kampuni ndogo na zenye ukubwa wa kati zitakazoajiri wahitimu wa vyuo vikuu zitapewa ruzuku kwa mara moja. Kampuni za kitaifa zitaongeza nafasi za ajira kwa miaka miwili mfululizo.

  "Tutaunga mkono miradi ya uwekezaji na ya utafiti wa kisayansi kutoa nafasi ya kufundisha wanafunzi watakaohitimu, kwa wale waliosimamisha mafunzo kutokana na maambukizi ya virusi vya Corona wanaweza kuongeza muda wa kutoa ruzuku. Kampuni zikisaini mkataba na wahitimu wa vyuo vikuu ambavyo muda wao wa mafunzo bado haujakamilika, zitapongezwa na kupewa ruzuku ya mafunzo inayosalia. Wahitimu wanaoahirisha kuondoka kutoka vyuo vikuu, wataongezeka muda wa kusajili, kuwasilisha nyaraka na shughuli nyingine. "

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako