• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sekta mbalimbali za Marekani zapinga Trump kulegeza hatua za kupambana na virusi vya Corona

    (GMT+08:00) 2020-03-25 18:30:14

    Rais Donald Trump wa Marekani amesema, anafikiri kulegeza hatua za kupambana na virusi vya Corona kutokana na athari ya kiuchumi, kauli iliyopingwa vikali na sekta mbalimbali za Marekani.

    Spika wa bunge la Marekani Bibi Nancy Pelosi amesema, ni bora rais Trump asikilize zaidi pendekezo la wanasayansi na kusema maneno ya kuheshimu sayansi. Pia amesema, uchumi wa Marekani utafufuka baada ya kumalizika kwa mlipuko huo.

    Kauli hiyo ya Bi. Pelosi imeungwa mkono na mgombea wa urais wa Chama cha Demokrasia cha Marekani Bw. Joe Biden ambaye amesema, ni bora rais Trump aache kuongea na kusilikiza zaidi maoni ya madaktari.

    Mwanzilishi wa kampuni ya Microsoft Bw. Bill Gates amesema, haifai kurudisha shughuli za kawaida za kiuchumi katika kipindi hiki cha kuenea kwa virusi, na njia pekee sahihi ni kujitenga kwa wiki 6 hadi 10 ili kuzuia kwa kikamilifu kuenea kwa virusi hivyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako