• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Watekaji wataka mil. 120- kuachia wachezaji

  (GMT+08:00) 2020-03-25 18:30:38

  Watu wasiojulikana wameendelea kuwashikilia wanasoka wawili wa klabu za Enyimba FC na Abia Comet, na ujumbe wao ni kwamba wanataka wapewe Naira milioni 20 ambazo ni zaidi ya Sh mil. 120 za Tanzania ndipo wawaachie. Wachezaji waliotekwa ni Dayo Ojo wa Enyimba FC inayocheza Ligi Kuu, wakati mwenzake ni Benjamin Iluyomade anayeichezea Abia Comet inayoshiriki Ligi Daraja la Pili. Aidha, tukio la kutekwa kwa nyota hao lilitokea Jumapili jioni katika moja ya mitaa ya Jimbo la Ondo. Taarifa ya watekaji kutaka kiasi hicho cha fedha imetolewa na mmoja kati ya ndugu wa wachezaji hao, ambaye hata hivyo alikataa jina lake kuwekwa hadharani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako